1 Wafalme Chapter 17

For English

Read 1 Wafalme Chapter 17 Online

Read 1 Wafalme Chapter 17 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wafalme in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Wafalme and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Wafalme 17

Sura 17

1. Basi Eliya Mtishbi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu, Kama Bwana, Mungu wa Israeli, aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na umande wala mvua miaka hii, ila kwa neno langu.

2. Neno la Bwana likamjia, kusema,

3. Ondoka hapa, geuka, uende upande wa mashariki, ujifiche karibu na kijito cha Kerithi kinachokabili Yordani.

4. Itakuwa utakunywa maji ya kile kijito; nami nimewaamuru kunguru wakulishe huko.

5. Basi akaenda akafanya kama alivyosema Bwana; kwa kuwa akaenda akakaa karibu na kijito cha Kerithi, kinachokabili Yordani.

6. Kunguru wakamletea mkate na nyama asubuhi, na mkate na nyama jioni, akanywa maji ya kile kijito.

7. Ikawa, baada ya siku kupita, kile kijito kikakatika, kwa sababu mvua haikunyesha katika nchi.

8. Neno la Bwana likamjia, kusema,

9. Ondoka, uende Sarepta, ulio mji wa Sidoni, ukae huko. Tazama, nimemwagiza mwanamke mjane wa huko akulishe.

10. Basi, akaondoka, akaenda Sarepta; hata alipofika langoni pa mji, kumbe! Mwanamke mjane alikuwako akiokota kuni; akamwita, akamwambia, Niletee, nakuomba, maji kidogo chomboni nipate kunywa.

11. Alipokuwa akienda kuleta, akamwita akasema, Niletee, nakuomba, kipande cha mkate mkononi mwako.

12. Naye akasema, Kama Bwana, Mungu wako, aishivyo, sina mkate, ila konzi ya unga katika pipa, na mafuta kidogo katika chupa; nami ninaokota kuni mbili ili niingie nijipikie nafsi yangu na mwanangu, tuule tukafe.

13. Eliya akamwambia, Usiogope; enenda ukafanye kama ulivyosema; lakini unifanyie kwanza mkate mdogo ukaniletee; kisha ujifanyie nafsi yako na mwanao.

14. Kwa kuwa Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Lile pipa la unga halitapunguka, wala ile chupa ya mafuta haitaisha, hata siku ile Bwana atakapoleta mvua juu ya nchi.

15. Basi akaenda, akafanya kama alivyosema Eliya; na yeye mwenyewe, na Eliya, na nyumba yake, wakala siku nyingi.

16. Lile pipa la unga halikupunguka, wala ile chupa ya mafuta haikuisha, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa kinywa cha Eliya.

17. Ikawa, baada ya hayo, mwana wake yule mwanamke, bibi wa nyumba ile, akaugua; ugonjwa wake ukazidi hata akawa hana pumzi tena.

18. Akamwambia Eliya, Nina nini nawe, Ee mtu wa Mungu? Je! Umenijia ili dhambi yangu ikumbukwe, ukamwue mwanangu?

19. Akamwambia, Nipe mwanao. Akamtoa katika kifua chake, akamchukua juu chumbani mle alimokaa mwenyewe, akamlaza kitandani pake.

20. Akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, je! Umemtenda mabaya mjane huyu ninayekaa kwake hata kumfisha mwanawe.

21. Akajinyosha juu ya mtoto mara tatu, akamwomba Bwana, akanena, Ee Bwana, Mungu wangu, nakusihi, roho ya mtoto huyu imrudie ndani yake tena.

22. Bwana akaisikia sauti ya Eliya; na roho ya mtoto ikamrudia, akafufuka.

23. Eliya akamtwaa mtoto, akamchukua toka orofani mpaka chini ya nyumba ile, akampa mama yake. Eliya akanena, Tazama, mwanao yu hai.

24. Mwanamke akamwambia Eliya, Sasa najua ya kuwa wewe ndiwe mtu wa Mungu, na ya kuwa neno la Bwana kinywani mwako ni kweli.

About 1 Wafalme Chapter 17

Read 1 Wafalme Chapter 17 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wafalme in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Wafalme
Chapter: 17
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Wafalme. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Wafalme Chapter 17 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Wafalme Chapter 17?

1 Wafalme Chapter 17 is part of the Book of 1 Wafalme in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Wafalme Chapter 17 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-wafalme

  1. 1 Wafalme Chapter 3
  2. 1 Wafalme Chapter 14
  3. 1 Wafalme Chapter 1
  4. 1 Wafalme Chapter 21
  5. 1 Wafalme Chapter 12
  6. 1 Wafalme Chapter 11
  7. 1 Wafalme Chapter 10

Explore More from Agano la Kale

  1. 2 Samweli Chapter 24
  2. 2 Wafalme Chapter 11
  3. Zaburi Chapter 36
  4. Ezekieli Chapter 25
  5. Isaya Chapter 57
  6. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 13
  7. Ayubu Chapter 30

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 135
  2. Ezekieli Chapter 13
  3. 1 Samweli Chapter 21
  4. Warumi Chapter 5
  5. 2 Samweli Chapter 19
  6. Yeremia Chapter 19
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 17
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *