1 Wathesalonike Chapter 2

For English

Read 1 Wathesalonike Chapter 2 Online

Read 1 Wathesalonike Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wathesalonike in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 1 Wathesalonike and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1 Wathesalonike 2

Sura 2

1. Maana ninyi wenyewe, ndugu, mwakujua kuingia kwetu kwenu, ya kwamba hakukuwa bure;

2. lakini tukiisha kuteswa kwanza na kutendwa jeuri, kama mjuavyo, katika Filipi, twalithubutu katika Mungu kuinena Injili ya Mungu kwenu, kwa kuishindania sana.

3. Kwa maana maonyo yetu siyo ya ukosefu, wala ya uchafu, wala ya hila;

4. bali kama vile tulivyopata kibali kwa Mungu tuwekewe amana Injili, ndivyo tunenavyo; si kama wapendezao wanadamu, bali wampendezao Mungu anayetupima mioyo yetu.

5. Maana hatukuwa na maneno ya kujipendekeza wakati wo wote, kama mjuavyo, wala maneno ya juujuu ya kuficha choyo; Mungu ni shahidi.

6. Hatukutafuta utukufu kwa wanadamu, wala kwenu, wala kwa wengine tulipokuwa tukiweza kuwalemea kama mitume wa Kristo;

7. bali tulikuwa wapole katikati yenu, kama vile mlezi awatunzavyo watoto wake mwenyewe.

8. Vivyo hivyo nasi tukiwatumaini kwa upendo mwingi, tuliona furaha kuwapa, si Injili ya Mungu tu, bali na roho zetu pia, kwa sababu mmekuwa wapendwa wetu.

9. Maana, ndugu, mnakumbuka taabu yetu na masumbufu yetu; kwa kuwa mchana na usiku tulifanya kazi tusije tukamlemea mtu wa kwenu awaye yote, tukawahubiri hivi Injili ya Mungu.

10. Ninyi ni mashahidi, na Mungu pia, jinsi tulivyokaa kwenu ninyi mnaoamini, kwa utakatifu, na kwa haki, bila kulaumiwa;

11. vile vile, kama mjuavyo, jinsi tulivyomwonya kila mmoja wenu kama baba awaonyavyo watoto wake mwenyewe, tukiwatia moyo na kushuhudia;

12. ili mwenende kama ilivyo wajibu wenu kwa Mungu, mwenye kuwaita ninyi ili mwingie katika ufalme wake na utukufu wake.

13. Kwa sababu hiyo sisi nasi twamshukuru Mungu bila kukoma, kwa kuwa, mlipopata lile neno la ujumbe la Mungu mlilolisikia kwetu, mlilipokea si kama neno la wanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli; litendalo kazi pia ndani yenu ninyi mnaoamini.

14. Maana ninyi, ndugu, mlikuwa wafuasi wa makanisa ya Mungu yaliyo katika Uyahudi, katika Kristo Yesu; kwa kuwa mlipata mateso yale yale kwa watu wa taifa lenu wenyewe, waliyoyapata na hao kwa Wayahudi;

15. ambao walimwua Bwana Yesu, na hao manabii, na kutuudhi sisi; wala hawampendezi Mungu, wala hawapatani na watu wo wote;

16. huku wakituzuia tusiseme na Mataifa wapate kuokolewa; ili watimize dhambi zao siku zote. Lakini hasira imewafikia hata mwisho.

17. Lakini sisi, ndugu, tukiwa tumefarakana nanyi kwa kitambo, kwa uso si kwa moyo, tulizidi kutamani kwa shauku nyingi kuwaona nyuso zenu.

18. Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia.

19. Maana tumaini letu, au furaha yetu, au taji ya kujionea fahari, ni nini? Je! Si ninyi, mbele za Bwana wetu Yesu, wakati wa kuja kwake?

20. Maana ninyi ndinyi utukufu wetu, na furaha yetu.

About 1 Wathesalonike Chapter 2

Read 1 Wathesalonike Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 1 Wathesalonike in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 1 Wathesalonike
Chapter: 2
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 1 Wathesalonike. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 1 Wathesalonike Chapter 2 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 1 Wathesalonike Chapter 2?

1 Wathesalonike Chapter 2 is part of the Book of 1 Wathesalonike in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 1 Wathesalonike Chapter 2 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 1-wathesalonike

  1. 1 Wathesalonike Chapter 4
  2. 1 Wathesalonike Chapter 3
  3. 1 Wathesalonike Chapter 1
  4. 1 Wathesalonike Chapter 5

Explore More from Agano Jipya

  1. Waefeso Chapter 3
  2. Ufunuo wa Yohana Chapter 11
  3. Mathayo Chapter 4
  4. Ufunuo wa Yohana Chapter 8
  5. Yohana Chapter 11
  6. 1 Petro Chapter 5
  7. Marko Chapter 6

Related Chapters & Readings

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 27
  2. Mambo ya Walawi Chapter 9
  3. Amosi Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 2
  5. Mwanzo Chapter 49
  6. 1 Wakorintho Chapter 15
  7. Yeremia Chapter 24
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *