2 Mambo ya Nyakati Chapter 8

For English

Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 8 Online

Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 8 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Mambo ya Nyakati and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

2 Mambo ya Nyakati 8

Sura 8

1. Ikawa miaka ishirini ilipopita, ambayo katika hiyo Sulemani aliijenga nyumba ya Bwana, na nyumba yake mwenyewe;

2. ndipo Sulemani akaijenga miji ile Hiramu aliyompa Sulemani, akawakalisha humo wana wa Israeli.

3. Naye Sulemani akaenda Hamath-zoba, akaushinda.

4. Akaujenga Tadmori wa nyikani, na miji yote ya hazina, aliyoijenga katika Hamathi.

5. Tena akaujenga Beth-horoni wa juu, na Beth-horoni wa chini, miji yenye boma, yenye kuta, na malango, na makomeo;

6. na Baalathi, na miji yote ya hazina Sulemani aliyokuwa nayo, na miji yote ya magari yake, na miji ya wapanda farasi wake, na ya anasa yote aliyopenda Sulemani kujenga humo Yerusalemu, na katika Lebanoni, na katika nchi yote ya mamlaka yake.

7. Basi kwa habari ya watu wote waliosalia wa Wahiti, na wa Waamori, na wa Waperizi, na wa Wahivi, na wa Wayebusi, wasiokuwa wa Israeli;

8. wa watoto wao waliosalia baada yao katika nchi, ambao wana wa Israeli hawakuwakomesha, katika hao Sulemani akawatumikisha shokoa hata leo.

9. Wala katika wana wa Israeli Sulemani hakuwafanya watumwa kazini mwake; lakini hao walikuwa watu wa vita, na wakuu wa majemadari wake, na maakida wa magari yake na wa wapanda farasi wake.

10. Na hao walikuwa maakida wakuu wa Sulemani, watu mia mbili na hamsini, waliotawala juu ya watu.

11. Sulemani akamleta binti Farao kutoka mji wa Daudi mpaka nyumba aliyomjengea; kwa kuwa alisema, Mke wangu hatakaa nyumbani mwa Daudi mfalme wa Israeli, kwa kuwa ni patakatifu, mahali palipofika sanduku la Bwana.

12. Ndipo Sulemani akamtolea Bwana sadaka za kuteketezwa juu ya madhabahu ya Bwana, aliyoijenga mbele ya ukumbi,

13. kadiri ilivyohitajiwa huduma ya kila siku, akitoa sawasawa na amri ya Musa, siku za sabato, na za mwezi mpya, na za sikukuu zilizoamriwa, mara tatu kila mwaka, yaani, sikukuu ya mikate isiyochachwa, na sikukuu ya majuma, na sikukuu ya vibanda.

14. Akaziamuru, sawasawa na agizo la Daudi babaye, zamu za makuhani za kutumika, nao Walawi kwa kadiri ya malinzi yao, ili kusifu, na kuhudumu mbele ya makuhani, kama ilivyohitajiwa kila siku; tena mabawabu kwa zamu zao za kila mlango; maana ndivyo alivyoamuru Daudi mtu wa Mungu.

15. Wala hawakuyaacha maagizo ya mfalme aliyowaamuru makuhani na Walawi kwa neno lo lote, wala kwa habari ya hazina.

16. Basi ikatengenezwa kazi yote ya Sulemani hata siku ya kutiwa msingi wa nyumba ya Bwana, na hata ilipokwisha. Hivyo ikamalizika nyumba ya Bwana.

17. Ndipo Sulemani akaenda Esion-geberi, na Elothi, pwani ya nchi ya Edomu.

18. Naye Hiramu akamletea merikebu kwa mikono ya watumishi wake, na watumishi waliokuwa wana-maji; nao wakafika Ofiri pamoja na watumishi wa Sulemani, wakachukua kutoka huko talanta mia nne na hamsini za dhahabu, wakamletea mfalme Sulemani.

About 2 Mambo ya Nyakati Chapter 8

Read 2 Mambo ya Nyakati Chapter 8 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: 2 Mambo ya Nyakati
Chapter: 8
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Mambo ya Nyakati. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading 2 Mambo ya Nyakati Chapter 8 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is 2 Mambo ya Nyakati Chapter 8?

2 Mambo ya Nyakati Chapter 8 is part of the Book of 2 Mambo ya Nyakati in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete 2 Mambo ya Nyakati Chapter 8 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from 2 MambO Ya Nyakati

  1. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 21
  2. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 17
  3. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 13
  4. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 12
  5. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 5
  6. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 4
  7. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 35

Explore More from Agano la Kale

  1. Ezra Chapter 2
  2. Mithali Chapter 12
  3. Sefania Chapter 1
  4. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 25
  5. Isaya Chapter 45
  6. Yona Chapter 4
  7. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 4

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 94
  2. Ayubu Chapter 31
  3. Zaburi Chapter 10
  4. Hesabu Chapter 22
  5. Zaburi Chapter 89
  6. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 23
  7. Ayubu Chapter 6
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *