Hesabu Chapter 12

For English

Read Hesabu Chapter 12 Online

Read Hesabu Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Hesabu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Hesabu and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Hesabu 12

Sura 12

1. Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.

2. Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao.

3. Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.

4. Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.

5. Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.

6. Kisha akawaambia, Sikizeni basi maneno yangu; Akiwapo nabii kati yenu, Mimi, Bwana, nitajifunua kwake katika maono, Nitasema naye katika ndoto.

7. Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;

8. Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?

9. Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.

10. Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe kama theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.

11. Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.

12. Nakusihi, asiwe kama mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake.

13. Musa akamlilia Bwana, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana.

14. Bwana akamwambia Musa, Je! Kama baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena.

15. Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena.

16. Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapanga kambi katika nyika ya Parani.

About Hesabu Chapter 12

Read Hesabu Chapter 12 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Hesabu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Hesabu
Chapter: 12
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Hesabu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Hesabu Chapter 12 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Hesabu Chapter 12?

Hesabu Chapter 12 is part of the Book of Hesabu in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Hesabu Chapter 12 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from Hesabu

  1. Hesabu Chapter 22
  2. Hesabu Chapter 20
  3. Hesabu Chapter 35
  4. Hesabu Chapter 7
  5. Hesabu Chapter 31
  6. Hesabu Chapter 26
  7. Hesabu Chapter 25

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 39
  2. Zaburi Chapter 119
  3. Mambo ya Walawi Chapter 19
  4. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 24
  5. Kumbukumbu la Torati Chapter 7
  6. Hesabu Chapter 23
  7. Ufunuo wa Yohana Chapter 12
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *