Read Hesabu Chapter 27 Online
Read Hesabu Chapter 27 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Hesabu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Hesabu and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Hesabu 27
Sura 27
1. Wakati huo wakakaribia hao binti za Selofehadi, mwana wa Heferi, mwana wa Gileadi, mwana wa Makiri, mwana wa Manase, wa jamaa za Manase mwana wa Yusufu; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya; Mala, na Noa, na Hogla, na Milka, na Tirsa.
2. Nao wakasimama mbele ya Musa, na mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya wakuu, na mkutano wote, mlangoni pa hema ya kukutania, wakasema,
3. Babaetu alikufa nyikani, naye hakuwamo katika mkutano wa hao waliojikutanisha kinyume cha Bwana katika mkutano wa Kora; lakini akafa katika dhambi zake mwenyewe; naye alikuwa hana wana wa kiume.
4. Kwa nini basi jina la babaetu kufutwa katika jamaa zake kwa sababu alikuwa hana mwana wa kiume? Tupe sisi urithi pamoja na ndugu zake babaetu.
5. Basi Musa akaleta neno lao mbele ya Bwana
6. Bwana akanena na Musa, na kumwambia,
7. Hao binti za Selofehadi wananena lililo haki; kweli utawapa milki ya urithi pamoja na ndugu za baba yao; nawe utawapa urithi wa baba yao.
8. Kisha utanena na wana wa Israeli, na kuwaambia, Mtu akifa, naye hana mwana wa kiume, ndipo utampa binti yake urithi wake.
9. Tena ikiwa hana binti, mtawapa nduguze urithi wake.
10. Na ikiwa hana ndugu, mtawapa ndugu za babaye huo urithi wake.
11. Tena ikiwa babaye hana ndugu, utampa huyo aliye karibu naye katika jamaa zake huo urithi wake, naye atakuwa nao; na neno hili litakuwa ni amri ya hukumu kwa wana wa Israeli, kama Bwana alivyomwagiza Musa.
12. Bwana akamwambia Musa, Panda wewe juu ya mlima huu wa Abarimu, uitazame nchi niliyowapa wana wa Israeli.
13. Na ukiisha kuiona, wewe nawe utakusanyika pamoja na baba zako, kama Haruni ndugu yako alivyokusanyika;
14. kwa sababu mliasi juu ya neno langu katika jangwa la Sini wakati wa mateto ya mkutano, wala hamkunistahi, hapo majini, mbele ya macho yao. (Maji hayo ndiyo maji ya Meriba ya Kadeshi katika jangwa la Sini.)
15. Musa akanena na Bwana akisema,
16. Bwana, Mungu wa roho za wenye mwili wote, na aweke mtu juu ya mkutano,
17. atakayetoka mbele yao, na kuingia mbele yao; atakayewaongoza watokapo, na kuwaleta ndani; ili mkutano wa Bwana wasiwe kama kondoo wasio na mchungaji.
18. Bwana akamwambia Musa, Mtwae Yoshua, mwana wa Nuni, mtu mwenye roho ndani yake, ukamwekee mkono wako;
19. kisha ukamweke mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wote; ukampe mausia mbele ya macho yao.
20. Nawe utaweka juu yake sehemu ya heshima yako, ili mkutano wote wa wana wa Israeli wapate kutii.
21. Naye atasimama mbele ya Eleazari kuhani, naye atamwulizia kwa hukumu ya ile Urimu mbele za Bwana; kwa neno lake watatoka, na kwa neno lake wataingia; yeye na wana wa Israeli wote pamoja naye, mkutano wote pia.
22. Musa akafanya kama Bwana alivyomwamuru; akamtwaa Yoshua, akamweka mbele ya Eleazari kuhani, na mbele ya mkutano wote;
23. kisha akaweka mikono yake juu yake, akampa mausia, kama Bwana alivyosema kwa mkono wa Musa.
About Hesabu Chapter 27
Read Hesabu Chapter 27 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Hesabu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Hesabu
Chapter: 27
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Hesabu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Hesabu Chapter 27 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Hesabu Chapter 27?
Hesabu Chapter 27 is part of the Book of Hesabu in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Hesabu Chapter 27 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Isaya Chapter 1
- Isaya Chapter 2
- Isaya Chapter 6
- Isaya Chapter 3
- Isaya Chapter 5
- Isaya Chapter 7
- Isaya Chapter 16
Explore More from Hesabu
- Hesabu Chapter 35
- Hesabu Chapter 20
- Hesabu Chapter 12
- Hesabu Chapter 17
- Hesabu Chapter 18
- Hesabu Chapter 30
- Hesabu Chapter 3