Hesabu Chapter 30

For English

Read Hesabu Chapter 30 Online

Read Hesabu Chapter 30 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Hesabu in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Hesabu and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Hesabu 30

Sura 30

1. Kisha Musa akanena na wale vichwa vya kabila za wana wa Israeli, na kuwaambia, Neno hili ndilo aliloliagiza Bwana.

2. Mtu atakapomwekea Bwana nadhiri, au, atakapoapa kiapo ili kufunga nafsi yake kwa kifungo, asilitangue neno lake; atafanya sawasawa na hayo yote yamtokayo kinywani mwake.

3. Tena mtu mke atakapomwekea Bwana nadhiri, na kufunga nafsi yake kwa kifungo, naye aketi katika nyumba ya babaye, katika ujana wake;

4. babaye naye akasikia nadhiri yake, na kile kifungo chake alichofungia nafsi yake, na babaye akamnyamazia; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichofungia nafsi yake kitathibitika.

5. Lakini kama huyo babaye akimkataza siku hiyo aliyosikia; nadhiri zake ziwazo zote, wala vifungo vyake alivyoifungia nafsi yake havitathibitika; na Bwana atamsamehe, kwa kuwa babaye alimkataza.

6. Tena kama amekwisha kuolewa na mume, wakati huo wa nadhiri zake, au wa neno hilo alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia;

7. na mumewe akasikia, naye akamnyamazia siku hiyo aliyosikia neno hilo; ndipo nadhiri zake zitathibitika, na vile vifungo ambavyo ameifunga nafsi yake vitathibitika.

8. Lakini kama mumewe akimkataza siku hiyo aliyolisikia; ndipo ataitangua nadhiri yake iliyo juu yake na neno alilolitamka kwa midomo yake pasipo kufikiri, alilojifungia; na Bwana atamsamehe

9. Lakini nadhiri ya mjane, au ya mwanamke aliyeachishwa mume, kila neno ambalo ameifunga nafsi yake kwalo, litathibitika juu yake.

10. Tena kama aliweka nadhiri nyumbani mwa mumewe, au kama aliifunga nafsi yake kwa kifungo pamoja na kiapo,

11. na mumewe alisikia akamnyamazia, wala hakumkataza; ndipo nadhiri zake zote zitathibitika, na kila kifungo alichojifungia kitathibitika.

12. Lakini kama mumewe alizibatilisha na kuzitangua siku hiyo aliyozisikia, ndipo kila neno lililotoka midomoni mwake katika hizo nadhiri zake, au katika kile kifungo cha nafsi yake, halitathibitika; huyo mumewe amezitangua; na Bwana atamsamehe.

13. Kila nadhiri, na kila kiapo kifungacho, ili kuitaabisha nafsi ya mwanamke mumewe aweza kuthibitisha, au mumewe aweza kutangua.

14. Lakini mumewe akimnyamazia mkewe kabisa siku hata siku ndipo azithibitisha nadhiri zote za mkewe, au vifungo vyake vyote vilivyo juu yake; yeye amezithibitisha, kwa kuwa alimnyamazia mkewe siku hiyo aliyozisikia nadhiri zake.

15. Lakini akizibatilisha na kuzitangua baada ya kuzisikia; ndipo yeye atachukua uovu wa mkewe.

16. Hizi ndizo amri, ambazo Bwana alimwagiza Musa, kati ya mtu mume na mkewe, kati ya baba na binti yake, katika ujana wake, ali nyumbani mwa babaye.

About Hesabu Chapter 30

Read Hesabu Chapter 30 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Hesabu in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Hesabu
Chapter: 30
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Hesabu. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Hesabu Chapter 30 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Hesabu Chapter 30?

Hesabu Chapter 30 is part of the Book of Hesabu in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Hesabu Chapter 30 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. 1 Samweli Chapter 1
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from Hesabu

  1. Hesabu Chapter 19
  2. Hesabu Chapter 16
  3. Hesabu Chapter 15
  4. Hesabu Chapter 4
  5. Hesabu Chapter 14
  6. Hesabu Chapter 23
  7. Hesabu Chapter 2

Related Chapters & Readings

  1. Kutoka Chapter 32
  2. 2 Wakorintho Chapter 12
  3. 1 Wafalme Chapter 5
  4. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 14
  5. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 22
  6. Waamuzi Chapter 8
  7. 2 Wafalme Chapter 19
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *