Read 2 Wafalme Chapter 24 Online
Read 2 Wafalme Chapter 24 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wafalme in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of 2 Wafalme and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
2 Wafalme 24
Sura 24
1. Katika siku zake akakwea Nebukadreza, mfalme wa Babeli na Yehoyakimu akawa mtumishi wake muda wa miaka mitatu; kisha , akageuka, akamwasi.
2. Naye Bwana akatuma juu yake vikosi vya Wakaldayo, na vikosi vya Washami, na vikosi vya Wamoabi, na vikosi vya wana wa Amoni, akawatuma juu ya Yuda ili kuiharibu, sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa mkono wa watumishi wake manabii.
3. Hakika kwa amri ya Bwana mambo hayo yalimpata Yuda, ili waondoshwe kutoka machoni pake, kwa sababu ya dhambi zake Manase, kadiri ya yote aliyoyafanya;
4. tena kwa ajili ya damu zisizo na hatia alizozimwaga; kwani aliujaza Yerusalemu damu zisizo na hatia; wala Bwana hakukubali kusamehe.
5. Basi mambo yote ya Yehoyakimu yaliyosalia, na yote aliyoyafanya, je! Hayakuandikwa katika kitabu-cha-tarehe cha wafalme wa Yuda?
6. Yehoyakimu akalala na babaze; na mwanawe Yekonia akatawala mahali pake.
7. Basi mfalme wa Misri hakuja tena kutoka nchi yake; kwa kuwa mfalme wa Babeli alikuwa amemnyang'anya nchi, tangu kijito cha Misri mpaka mto wa Frati, yote aliyokuwa nayo mfalme wa Misri.
8. Yekonia alikuwa na umri wa miaka kumi na minane alipoanza kutawala; akatawala miezi mitatu katika Yerusalemu; na jina la mama yake aliitwa Nehushta binti Elnathani wa Yerusalemu.
9. Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, mfano wa yote aliyoyafanya baba yake.
10. Wakati ule watumishi wa Nebukadreza mfalme wa Babeli wakakwea kwenda Yerusalemu, na mji ukahusuriwa.
11. Na Nebukadreza, mfalme wa Babeli, akaufikilia huo mji, hapo watumishi wake walipokuwa wakiuhusuru.
12. Na Yekonia, mfalme wa Yuda, akatoka akamwendea mfalme wa Babeli, yeye na mama yake, na watumishi wake, na wakuu wa watu wake, na maakida wake; mfalme wa Babeli akamchukua mateka katika mwaka wa nane wa kutawala kwake.
13. Akatoa huko hazina zote za nyumba ya Bwana, na hazina za nyumba ya mfalme, akavikata-kata vyombo vyote vya dhahabu ambavyo Sulemani, mfalme wa Israeli, alivifanya katika hekalu la Bwana, kama Bwana alivyosema.
14. Akawachukua mateka watu wa Yerusalemu wote pia, na wakuu wote, na mashujaa wote, watu elfu kumi; na mafundi wote, na wafua chuma wote; hapana mtu aliyebaki, ila waliokuwa wanyonge wa watu wa nchi.
15. Akamchukua Yekonia mpaka Babeli; na mama yake mfalme, na wake zake mfalme, na maakida wake, na wakuu wa nchi, aliwachukua mateka toka Yerusalemu mpaka Babeli.
16. Na mashujaa wote, watu elfu saba, na mafundi na wafua chuma elfu moja, wote pia wenye nguvu, tayari kwa vita, hao wote mfalme wa Babeli aliwachukua mateka mpaka Babeli.
17. Mfalme wa Babeli akamtawaza Matania, ndugu ya baba yake, awe mfalme badala yake, akalibadili jina lake, akamwita Sedekia.
18. Sedekia alikuwa na umri wa miaka ishirini na mmoja alipoanza kutawala; akatawala miaka kumi na mmoja katika Yerusalemu; na jina la mamaye aliitwa Hamutali, binti Yeremia wa Libna.
19. Akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, sawasawa na yote aliyoyafanya Yehoyakimu.
20. Maana kwa sababu ya hasira ya Bwana mambo hayo yalitokea katika Yerusalemu na katika Yuda, hata alipokuwa amewaondosha wasiwe mbele ya uso wake; naye Sedekia akamwasi mfalme wa Babeli.
About 2 Wafalme Chapter 24
Read 2 Wafalme Chapter 24 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of 2 Wafalme in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: 2 Wafalme
Chapter: 24
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading 2 Wafalme. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading 2 Wafalme Chapter 24 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is 2 Wafalme Chapter 24?
2 Wafalme Chapter 24 is part of the Book of 2 Wafalme in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete 2 Wafalme Chapter 24 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from 2-wafalme
- 2 Wafalme Chapter 2
- 2 Wafalme Chapter 14
- 2 Wafalme Chapter 5
- 2 Wafalme Chapter 1
- 2 Wafalme Chapter 7
- 2 Wafalme Chapter 12
- 2 Wafalme Chapter 18
Explore More from Agano la Kale
- Nahumu Chapter 3
- Mithali Chapter 18
- 1 Mambo ya Nyakati Chapter 22
- 1 Samweli Chapter 20
- Kumbukumbu la Torati Chapter 34
- Ayubu Chapter 32
- Isaya Chapter 25