Mambo ya Walawi Chapter 2

For English

Read Mambo ya Walawi Chapter 2 Online

Read Mambo ya Walawi Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mambo ya Walawi in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mambo ya Walawi and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mambo ya Walawi 2

Sura 2

1. Na mtu atakapomtolea Bwana matoleo ya sadaka ya unga, matoleo yake yatakuwa ya unga mwembamba; naye ataumiminia mafuta, na kutia na ubani juu yake;

2. kisha atauleta kwa wana wa Haruni, hao makuhani; naye atatwaa konzi moja katika huo unga mwembamba, na katika mafuta yake, na huo ubani wote; kisha kuhani atauteketeza kuwa ndio ukumbusho wake juu ya madhabahu, ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana;

3. na huo uliosalia wa ile sadaka ya unga utakuwa ni wa Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.

4. Tena, utakapotoa matoleo ya sadaka ya unga uliookwa tanuuni, yatakuwa mikate isiyotiwa chachu, ya unga mwembamba uliokandwa na mafuta, au maandazi yasiyochachwa yaliyopakwa mafuta.

5. Tena matoleo yako kwamba ni sadaka ya unga wa kaangoni, yatakuwa ya unga mwembamba usiotiwa chachu, uliokandwa na mafuta.

6. Utaukata-kata vipande, na kutia mafuta juu yake; ni sadaka ya unga.

7. Tena matoleo yako kwamba ni sadaka ya unga ya chunguni, yataandaliwa kwa unga mwembamba pamoja na mafuta.

8. Nawe utamletea Bwana sadaka ya unga iliyofanywa ya vitu hivyo; nayo italetwa kwa kuhani, naye ndiye atakayeisongeza madhabahuni.

9. Kisha kuhani atatwaa humo huo ukumbusho wa sadaka ya unga, naye atauteketeza juu ya madhabahu; ni kafara ya kusongezwa kwa njia ya moto, ya harufu ya kupendeza kwa Bwana.

10. Na hicho kitakachosalia katika sadaka ya unga kitakuwa cha Haruni na wanawe; ni kitu kitakatifu sana katika sadaka zilizosongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.

11. Sadaka ya unga iwayo yote itakayosongezwa kwa Bwana isitiwe chachu kabisa; kwa kuwa hamtateketeza chachu, wala asali iwayo yote, kuwa ni sadaka ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.

12. Vitu hivyo mtavisongeza kwa Bwana kuwa ni malimbuko; lakini visifike juu ya madhabahu kuwa ni harufu ya kupendeza.

13. Tena, kila toleo la sadaka yako ya unga utalitia chumvi; wala usiiache sadaka yako ya unga kupungukiwa na chumvi ya agano la Mungu wako; utatoa chumvi pamoja na matoleo yako yote.

14. Nawe kwamba wamtolea Bwana sadaka ya unga ya malimbuko, utatoa hiyo ngano katika masuke yake iliyochomwa motoni, ngano iliyopondwa ya masuke mabichi, ndiyo utakayoleta kuwa sadaka ya unga ya malimbuko yako.

15. Nawe utatia mafuta juu yake, na kuweka ubani juu yake; ni sadaka ya unga.

16. Huyo kuhani atauteketeza ukumbusho wake, yaani, sehemu ya ngano iliyopondwa ya hiyo sadaka, na sehemu ya mafuta yake, pamoja na ule ubani wake wote; ni kafara ya kusongezwa kwa Bwana kwa njia ya moto.

About Mambo ya Walawi Chapter 2

Read Mambo ya Walawi Chapter 2 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mambo ya Walawi in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mambo ya Walawi
Chapter: 2
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mambo ya Walawi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mambo ya Walawi Chapter 2 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mambo ya Walawi Chapter 2?

Mambo ya Walawi Chapter 2 is part of the Book of Mambo ya Walawi in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mambo ya Walawi Chapter 2 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Ayubu Chapter 4
  6. Kutoka Chapter 11
  7. Kutoka Chapter 2

Explore More from mambo-ya-walawi

  1. Mambo ya Walawi Chapter 5
  2. Mambo ya Walawi Chapter 27
  3. Mambo ya Walawi Chapter 20
  4. Mambo ya Walawi Chapter 17
  5. Mambo ya Walawi Chapter 9
  6. Mambo ya Walawi Chapter 10
  7. Mambo ya Walawi Chapter 23

Related Chapters & Readings

  1. Mithali Chapter 21
  2. Isaya Chapter 37
  3. Yeremia Chapter 27
  4. Kumbukumbu la Torati Chapter 31
  5. 1 Samweli Chapter 30
  6. Ufunuo wa Yohana Chapter 7
  7. Zaburi Chapter 141
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *