Mambo ya Walawi Chapter 17

For English

Read Mambo ya Walawi Chapter 17 Online

Read Mambo ya Walawi Chapter 17 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mambo ya Walawi in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mambo ya Walawi and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mambo ya Walawi 17

Sura 17

1. Bwana akamwambia Musa, akisema,

2. Sema na Haruni, na wanawe, na wana wote wa Israeli, ukawaambie; Neno hili ndilo aliloliamuru Bwana, akisema,

3. Mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli atakayechinja ng'ombe, au mwana-kondoo, au mbuzi, ndani ya marago, au atakayemchinja nje ya marago,

4. wala hamleti mlangoni pa hema ya kukutania, ili amtoe kuwa matoleo kwa Bwana mbele ya hema ya Bwana; mtu huyo atahesabiwa kuwa ana hatia ya damu; amemwaga damu; na mtu huyo atakatiliwa mbali na watu wake;

5. ili kusudi wana wa Israeli walete sadaka zao, wazichinjazo mashambani, naam, wazilete kwa Bwana, mpaka mlango wa hema ya kukutania, kwa huyo kuhani, ili wazichinje ziwe sadaka za amani kwa Bwana.

6. Naye kuhani atainyunyiza damu yake juu ya madhabahu ya Bwana, mlangoni pa hema ya kukutania, na kuyateketeza mafuta yake, yawe harufu njema mbele za Bwana.

7. Wala hawatatoa tena sadaka zao kwa wale majini, ambao huwafuata ili wafanye uasherati nao. Sheria hii itakuwa sheria ya milele kwao, kizazi baada ya kizazi.

8. Nawe utawaambia, Mtu awaye yote katika nyumba ya Israeli, au miongoni mwa wageni, wanaokaa nao, atoaye sadaka ya kuteketezwa au dhabihu,

9. wala haileti mlangoni pa hema ya kukutania, ili aisongeze kwa Bwana basi mtu huyo atatengwa na watu wake.

10. Kisha mtu awaye yote wa nyumba ya Israeli, au miongoni mwa hao wageni wakaao kati yao, atakayekula damu, ya aina yo yote, nitakunja uso wangu juu ya mtu huyo alaye damu, nami nitamkatilia mbali na watu wake.

11. Kwa kuwa uhai wa mwili u katika hiyo damu; nami nimewapa ninyi hiyo damu juu ya madhabahu, ili kufanya upatanisho kwa ajili ya nafsi zenu; kwani ni hiyo damu ifanyayo upatanisho kwa sababu ya nafsi.

12. Kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Hapana mtu miongoni mwenu aliye na ruhusa kula damu, wala mgeni aketiye kati yenu asile damu.

13. Mtu ye yote aliye wa wana wa Israeli, au wa hao wageni wakaao kati yenu, ambaye amemshika mnyama, au ndege ambaye huliwa, katika kuwinda kwake; atamwaga damu yake, na kuifunika mchanga.

14. Kwa maana kuliko huo uhai wa mnyama, hiyo damu yake ni moja na uhai wake; kwa hiyo naliwaambia wana wa Israeli, Msile damu ya mnyama wa aina yo yote; kwa kuwa uhai wa wanyama wote ni katika hiyo damu yake; atakayeila awaye yote atakatiliwa mbali.

15. Tena kila mtu atakayekula nyamafu, au nyama aliyeraruliwa na wanyama, kama ni mzalia, kama ni mgeni, atafua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hata jioni; ndipo atakapokuwa safi.

16. Lakini kwamba hazifui, wala haogi mwili, ndipo atakapochukua uovu wake.

About Mambo ya Walawi Chapter 17

Read Mambo ya Walawi Chapter 17 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mambo ya Walawi in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mambo ya Walawi
Chapter: 17
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mambo ya Walawi. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mambo ya Walawi Chapter 17 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mambo ya Walawi Chapter 17?

Mambo ya Walawi Chapter 17 is part of the Book of Mambo ya Walawi in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mambo ya Walawi Chapter 17 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Zaburi Chapter 1
  2. Habakuki Chapter 3
  3. Ayubu Chapter 1
  4. Zaburi Chapter 2
  5. Kutoka Chapter 11
  6. Kutoka Chapter 2
  7. Ayubu Chapter 4

Explore More from mambo-ya-walawi

  1. Mambo ya Walawi Chapter 11
  2. Mambo ya Walawi Chapter 4
  3. Mambo ya Walawi Chapter 19
  4. Mambo ya Walawi Chapter 2
  5. Mambo ya Walawi Chapter 8
  6. Mambo ya Walawi Chapter 16
  7. Mambo ya Walawi Chapter 22

Related Chapters & Readings

  1. Marko Chapter 2
  2. Zekaria Chapter 13
  3. Yohana Chapter 8
  4. Maombolezo Chapter 4
  5. Kumbukumbu la Torati Chapter 23
  6. Zaburi Chapter 137
  7. Hesabu Chapter 33
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *