Kutoka Chapter 31

For English

Read Kutoka Chapter 31 Online

Read Kutoka Chapter 31 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kutoka in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Kutoka and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Kutoka 31

Sura 31

1. Bwana akanena na Musa, na kumwambia,

2. Angalia, nimemwita kwa jina lake Bezaleli mwana wa Uri, mwana wa Huri, wa kabila ya Yuda;

3. nami nimemjaza roho ya Mungu, katika hekima, na maarifa, na ujuzi, na mambo ya kazi ya kila aina,

4. ili abuni kazi za ustadi, kuwa fundi wa dhahabu, na wa fedha, na wa shaba,

5. na kukata vito kwa kutiwa mahali, na kuchora miti, na kufanya kazi ya ustadi iwayo yote.

6. Tena, tazama, nimemchagua, awe pamoja naye, huyo Oholiabu, mwana wa Ahisamaki, wa kabila ya Dani; nami nimetia hekima katika mioyo ya wote wenye moyo wa hekima, ili wapate kufanya vyote nilivyokuagiza;

7. yaani, hema ya kukutania na sanduku la ushuhuda, na kiti cha rehema kilicho juu yake, na vyombo vyote vya Hema;

8. na meza, na vyombo vyake, na kinara cha taa safi pamoja na vyombo vyake vyote, na madhabahu ya kufukizia uvumba;

9. na madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake vyote, na birika na tako lake;

10. na mavazi yenye kufumwa kwa uzuri, na mavazi matakatifu ya Haruni kuhani, na mavazi ya wanawe, ili kutumika katika kazi ya ukuhani;

11. na mafuta ya kutiwa, na uvumba wa manukato mazuri, kwa ajili ya mahali patakatifu; sawasawa na yote niliyokuagiza ndivyo watakavyofanya wao.

12. Bwana akasema na Musa, na kumwambia,

13. Kisha, nena wewe na wana wa Israeli, na kuwaambia, Hakika mtazishika Sabato zangu, kwa kuwa ni ishara kati ya mimi na ninyi katika vizazi vyenu vyote; ili mpate kujua ya kuwa mimi ndimi Bwana niwatakasaye ninyi.

14. Basi mtaishika hiyo Sabato; kwa kuwa ni takatifu kwenu; kila mtu atakayeitia unajisi hakika yake atauawa; kwa kuwa kila mtu afanyaye kazi katika siku hiyo, nafsi hiyo itakatiliwa mbali na watu wake.

15. Kazi itafanywa siku sita; lakini siku ya saba ni Sabato ya kustarehe kabisa, takatifu kwa Bwana; kila mtu atakayefanya kazi yo yote katika siku ya Sabato, hakika yake atauawa.

16. Kwa ajili ya hayo wana wa Israeli wataishika Sabato, kuiangalia sana hiyo Sabato katika vizazi vyao vyote, ni agano la milele.

17. Ni ishara kati ya mimi na wana wa Israeli milele; kwani kwa siku sita Bwana alifanya mbingu na nchi, akastarehe kwa siku ya saba na kupumzika.

18. Hapo Bwana alipokuwa amekwisha zungumza na Musa katika mlima wa Sinai, akampa hizo mbao mbili za ushuhuda, mbao mbili za mawe, zilizoandikwa kwa chanda cha Mungu.

About Kutoka Chapter 31

Read Kutoka Chapter 31 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Kutoka in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Kutoka
Chapter: 31
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Kutoka. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Kutoka Chapter 31 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Kutoka Chapter 31?

Kutoka Chapter 31 is part of the Book of Kutoka in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Kutoka Chapter 31 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 2
  3. Isaya Chapter 6
  4. Isaya Chapter 3
  5. Isaya Chapter 7
  6. Isaya Chapter 14
  7. Isaya Chapter 8

Explore More from Kutoka

  1. Kutoka Chapter 22
  2. Kutoka Chapter 6
  3. Kutoka Chapter 25
  4. Kutoka Chapter 21
  5. Kutoka Chapter 17
  6. Kutoka Chapter 5
  7. Kutoka Chapter 20

Related Chapters & Readings

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 14
  2. 2 Wakorintho Chapter 4
  3. Zaburi Chapter 6
  4. 2 Wafalme Chapter 1
  5. Zaburi Chapter 2
  6. Mwanzo Chapter 27
  7. Isaya Chapter 59
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *