Filemoni Chapter 1

For English

Read Filemoni Chapter 1 Online

Read Filemoni Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Filemoni in the New Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Filemoni and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

1

Filemoni 1

Sura 1

1. Paulo, mfungwa wa Kristo Yesu, na Timotheo aliye ndugu yetu, kwa Filemoni mpendwa wetu, mtenda kazi pamoja nasi,

2. na kwa Afia, ndugu yetu, na kwa Arkipo askari mwenzetu, na kwa kanisa lililo katika nyumba yako.

3. Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu, Baba yetu, na kwa Bwana Yesu Kristo.

4. Namshukuru Mungu wangu sikuzote, nikikukumbuka katika maombi yangu;

5. nikisikia habari za upendo wako na imani uliyo nayo kwa Bwana Yesu na kwa watakatifu wote;

6. ili kwamba ushirika wa imani yako ufanye kazi yake, katika ujuzi wa kila kitu chema kilicho kwetu, katika Kristo.

7. Maana nalikuwa na furaha nyingi na faraja kwa sababu ya upendo wako, kwa kuwa mioyo ya watakatifu imeburudishwa nawe, ndugu yangu.

8. Kwa hiyo, nijapokuwa nina ujasiri katika Kristo kukuagiza likupasalo;

9. lakini, kwa ajili ya upendo nakusihi, kwa kuwa ni kama nilivyo, Paulo mzee, na sasa mfungwa wa Kristo Yesu pia.

10. Nakusihi kwa ajili ya mtoto wangu niliyemzaa katika vifungo vyangu, yaani, Onesimo;

11. ambaye zamani alikuwa hakufai, bali sasa akufaa sana, wewe na mimi pia;

12. niliyemtuma kwako, yeye mwenyewe, maana ni moyo wangu hasa;

13. ambaye mimi nalitaka akae kwangu, apate kunitumikia badala yako katika vifungo vya Injili.

14. Lakini sikutaka kutenda neno lo lote isipokuwa kwa shauri lako, ili kwamba wema wako usiwe kama kwa lazima, bali kwa hiari.

15. Maana, labda ndiyo sababu alitengwa nawe kwa muda, ili uwe naye tena milele;

16. tokea sasa, si kama mtumwa, bali zaidi ya mtumwa, ndugu mpendwa; kwangu mimi sana, na kwako wewe zaidi sana, katika mwili na katika Bwana.

17. Basi kama ukiniona mimi kuwa mshirika nawe, mpokee huyu kama mimi mwenyewe.

18. Na kama amekudhulumu, au unamwia kitu, ukiandike hicho juu yangu.

19. Mimi Paulo nimeandika kwa mkono wangu mwenyewe, mimi nitalipa. Sikuambii kwamba nakuwia hata nafsi yako.

20. Naam, ndugu yangu, nipate faida kwako katika Bwana; uniburudishe moyo wangu katika Kristo.

21. Kwa kuwa nakuamini kutii kwako ndiyo maana nimekuandikia, nikijua ya kuwa utafanya zaidi ya hayo nisemayo.

22. Na pamoja na hayo uniwekee tayari mahali pa kukaa; maana nataraji ya kwamba kwa maombi yenu mtajaliwa kunipata.

23. Epafra, aliyefungwa pamoja nami katika Kristo Yesu, akusalimu;

24. na Marko, na Aristarko, na Dema, na Luka, watendao kazi pamoja nami.

25. Neema ya Bwana Yesu Kristo na iwe pamoja na roho zenu.

About Filemoni Chapter 1

Read Filemoni Chapter 1 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Filemoni in the New Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Filemoni
Chapter: 1
Testament: New Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Filemoni. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Filemoni Chapter 1 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Filemoni Chapter 1?

Filemoni Chapter 1 is part of the Book of Filemoni in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Filemoni Chapter 1 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano Jipya

  1. Waebrania Chapter 1
  2. Waebrania Chapter 5
  3. Waebrania Chapter 6
  4. Waebrania Chapter 3
  5. Ufunuo wa Yohana Chapter 15
  6. Waebrania Chapter 4
  7. Waebrania Chapter 2

Explore More from Filemoni

Related Chapters & Readings

  1. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 10
  2. 2 Wafalme Chapter 21
  3. Zaburi Chapter 59
  4. Mhubiri Chapter 5
  5. Mwanzo Chapter 25
  6. Kumbukumbu la Torati Chapter 14
  7. 2 Mambo ya Nyakati Chapter 24
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *