Read Yeremia Chapter 19 Online
Read Yeremia Chapter 19 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yeremia in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Yeremia and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Yeremia 19
Sura 19
1. Bwana akasema hivi, Enenda ukanunue gudulia la mfinyanzi, ukachukue pamoja nawe baadhi ya wazee wa watu, na baadhi ya wazee wa makuhani;
2. ukatoke uende mpaka bonde la mwana wa Hinomu lililo karibu na mahali pa kuingia kwa lango la vigae, ukahubiri huko maneno nitakayokuambia,
3. ukisema, Lisikieni neno la Bwana, enyi wafalme wa Yuda, na wenyeji wa Yerusalemu; Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli asema hivi, Angalieni, nitaleta mabaya juu ya mahali hapa, ambayo mtu ye yote akisikia habari yake, masikio yake yatawaka.
4. Kwa sababu wameniacha mimi, nao wamepafanya mahali hapa kuwa mahali pageni, nao hapa wamewafukizia uvumba miungu mingine wasiowajua, wala wao, wala baba zao, wala wafalme wa Yuda; nao wamepajaza mahali hapa damu ya wasio na hatia;
5. nao wamemjengea Baali mahali pake palipo juu, ili kuwachoma moto wana wao, wawe sadaka za kuteketezwa kwa Baali; tendo nisiloliamuru mimi, wala kulinena, wala halikuingia moyoni mwangu;
6. basi, angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo katika siku hizo mahali hapa hapataitwa tena Tofethi, wala Bonde la mwana wa Hinomu, bali, Bonde la Machinjo.
7. Nami nitalitangua shauri la Yuda na Yerusalemu mahali hapa; nami nitawaangusha kwa upanga mbele za adui zao, na kwa mkono wa watu watafutao roho zao; na mizoga yao nitawapa ndege wa angani na wanyama wakali wa nchi, iwe chakula chao.
8. Nami nitaufanya mji huu kuwa kitu cha kushangaza watu, na kuzomewa; kila mtu apitaye karibu nao atashangaa, na kuzomea kwa sababu ya mapigo yake.
9. Nami nitawalazimisha kula nyama ya wana wao, na nyama ya binti zao, nao watakula kila mmoja nyama ya rafiki yake, wakati wa mazingira na dhiki, ambayo adui zao, na watu wale watafutao roho zao, watawadhiikisha.
10. Ndipo hapo utalivunja gudulia lile, mbele ya macho ya watu wale waendao pamoja nawe,
11. na kuwaambia, Bwana wa majeshi asema hivi, Hivyo ndivyo nitakavyowavunja watu hawa, na mji huu, kama mtu avunjavyo chombo cha mfinyanzi, kisichoweza kutengenezwa tena na kuwa kizima; nao watazika watu katika Tofethi hata hapatabaki mahali pa kuzika.
12. Hivyo ndivyo nitakavyopatenda mahali hapa, asema Bwana, nao wakaao humo, hata kufanya mji huu kuwa kama Tofethi;
13. na nyumba za Yerusalemu, na nyumba za wafalme wa Yuda, zilizotiwa unajisi, zitakuwa kama mahali pa Tofethi; naam, nyumba zote ambazo juu ya dari zake wamelifukizia uvumba jeshi lote la mbinguni, na kuwamiminia miungu mingine sadaka za kunywewa.
14. Kisha Yeremia akatoka huko Tofethi, huko ambako Bwana alimtuma atoe unabii; naye akasimama katika ua wa nyumba ya Bwana, akawaambia watu wote,
15. Bwana wa majeshi, Mungu wa Israeli, asema hivi, Tazama, nitaleta juu ya mji huu, na juu ya vijiji vyake vyote, mabaya yote niliyoyanena juu yake; kwa sababu wamefanya shingo zao kuwa ngumu, kusudi wasiyasikie maneno yangu.
About Yeremia Chapter 19
Read Yeremia Chapter 19 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Yeremia in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Yeremia
Chapter: 19
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Yeremia. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Yeremia Chapter 19 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Yeremia Chapter 19?
Yeremia Chapter 19 is part of the Book of Yeremia in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Yeremia Chapter 19 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
- Ayubu Chapter 4
Explore More from Yeremia
- Yeremia Chapter 22
- Yeremia Chapter 16
- Yeremia Chapter 4
- Yeremia Chapter 40
- Yeremia Chapter 26
- Yeremia Chapter 37
- Yeremia Chapter 1