Esta Chapter 3

For English

Read Esta Chapter 3 Online

Read Esta Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Esta in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Esta and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Esta 3

Sura 3

1. Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya maakida wote waliokuwapo pamoja naye.

2. Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia.

3. Basi watumishi wa mfalme walioketi mlangoni pa mfalme wakamwambia Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya mfalme?

4. Ikawa, waliposema naye kila siku asiwasikilize, wakamwarifu Hamani, ili kuona kama mambo yake Mordekai yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa yeye ni Myahudi.

5. Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana.

6. Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai.

7. Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari.

8. Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao.

9. Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme.

10. Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi.

11. Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema.

12. Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake.

13. Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara.

14. Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote wawe tayari siku ile ile.

15. Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika.

About Esta Chapter 3

Read Esta Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Esta in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Esta
Chapter: 3
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Esta. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Esta Chapter 3 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Esta Chapter 3?

Esta Chapter 3 is part of the Book of Esta in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Esta Chapter 3 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 3
  3. Isaya Chapter 2
  4. Isaya Chapter 6
  5. Isaya Chapter 7
  6. Isaya Chapter 14
  7. Isaya Chapter 5

Explore More from esta

  1. Esta Chapter 4
  2. Esta Chapter 2
  3. Esta Chapter 8
  4. Esta Chapter 7
  5. Esta Chapter 9
  6. Esta Chapter 5
  7. Esta Chapter 9

Related Chapters & Readings

  1. Zekaria Chapter 2
  2. Ezekieli Chapter 1
  3. 2 Wafalme Chapter 4
  4. Danieli Chapter 4
  5. Kumbukumbu la Torati Chapter 16
  6. Kutoka Chapter 4
  7. Ezekieli Chapter 5
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *