Read Wimbo Ulio Bora Chapter 6 Online
Read Wimbo Ulio Bora Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Wimbo Ulio Bora in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Wimbo Ulio Bora and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Wimbo Ulio Bora 6
Sura 6
1. Mpendwa wako amekwenda wapi, Wewe uliye mzuri katika wanawake? Mpendwa wako amegeukia upande upi, Ili tumtafute pamoja nawe?
2. Mpendwa wangu ameshukia bustani yake, Kwenye matuta ya rihani; Ili kulisha penye bustani, Ili kuchuma nyinyoro.
3. Mimi ni wake mpendwa wangu, naye ni wangu, Hulisha kundi lake penye nyinyoro.
4. Mpenzi wangu, u mzuri kama Tirza, Mwenye kupendeza kama Yerusalemu, Wa kutisha kama wenye bendera.
5. Uyageuzie macho yako mbali nami, Kwa maana yamenitisha sana. Nywele zako ni kama kundi la mbuzi, Wakijilaza mbavuni pa Gileadi.
6. Meno yako kama kundi la kondoo, Wakipanda kutoka kuoshwa; Ambao kila mmoja amezaa mapacha, Wala hakuna aliyefiwa kati yao.
7. Mashavu yako ni kama kipande cha komamanga, Nyuma ya barakoa yako.
8. Wako malkia sitini, na masuria themanini, Na wanawali wasiohesabika;
9. Hua wangu, mkamilifu wangu, ni mmoja tu, Mtoto wa pekee wa mamaye. Ndiye kipenzi chake aliyemzaa, Binti wakamwona wakamwita heri; Malkia na masuria nao wakamwona, Wakamsifu, wakisema,
10. Ni nani huyu atazamaye kama alfajiri, Mzuri kama mwezi, safi kama jua, Wa kutisha kama wenye bendera?
11. Nalishukia bustani ya milozi, Ili kuyatazama machipuko ya bondeni; Nione kama mzabibu umechanua, Kama mikomamanga imetoa maua.
12. Kabla sijajua, roho yangu ilinileta Katikati ya magari ya wakuu wangu.
13. Rudi, rudi, Mshulami, Rudi, rudi, ili sisi tukutazame.
About Wimbo Ulio Bora Chapter 6
Read Wimbo Ulio Bora Chapter 6 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Wimbo Ulio Bora in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Wimbo Ulio Bora
Chapter: 6
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Wimbo Ulio Bora. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Wimbo Ulio Bora Chapter 6 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Wimbo Ulio Bora Chapter 6?
Wimbo Ulio Bora Chapter 6 is part of the Book of Wimbo Ulio Bora in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Wimbo Ulio Bora Chapter 6 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- 1 Samweli Chapter 1
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
Explore More from wimbo-ulio-bora
- Wimbo Ulio Bora Chapter 1
- Wimbo Ulio Bora Chapter 4
- Wimbo Ulio Bora Chapter 5
- Wimbo Ulio Bora Chapter 7
- Wimbo Ulio Bora Chapter 3
- Wimbo Ulio Bora Chapter 2
- Wimbo Ulio Bora Chapter 8