Mhubiri Chapter 5

For English

Read Mhubiri Chapter 5 Online

Read Mhubiri Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mhubiri in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Mhubiri and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Mhubiri 5

Sura 5

1. Jitunze mguu wako uendapo nyumbani kwa Mungu; Maana ni heri kukaribia ili usikie, Kuliko kutoa kafara ya wapumbavu; Ambao hawajui kuwa wafanya mabaya.

2. Usiseme maneno ya ujinga kwa kinywa chako, wala moyo wako usiwe na haraka kunena mbele za Mungu; kwa maana, Mungu yuko mbinguni, na wewe upo chini, Kwa hiyo maneno yako na yawe machache.

3. Kwa maana ndoto huja kwa sababu ya shughuli nyingi; na sauti ya mpumbavu kwa njia ya wingi wa maneno.

4. Wewe ukimwekea Mungu nadhiri, usikawie kuiondoa; kwa kuwa yeye hawi radhi na wapumbavu; basi, uiondoe hiyo uliyoiweka nadhiri.

5. Ni afadhali usiweke nadhiri, Kuliko kuiweka usiiondoe.

6. Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba umepitiliwa; kwani Mungu akukasirikie sauti yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?

7. Maana ndivyo ilivyo katika habari za wingi wa ndoto, na ubatili, na maneno mengi; walakini wewe umche Mungu.

8. Ujapokuwa unaona maskini kuonewa, na hukumu na haki kuondolewa kwa jeuri katika jimbo, usilistaajabie jambo hilo; kwa sababu, Aliye juu kuliko walio juu huangalia; Tena wako walio juu kupita hao.

9. Lakini, pamoja na hayo, manufaa ya nchi kwa kila njia ni mfalme anayejibidiisha kwa ajili ya shamba.

10. Apendaye fedha hatashiba fedha, Wala apendaye wingi hatashiba maongeo. Hayo pia ni ubatili.

11. Mali yakiongezeka, hao walao nao waongezeka na mwenyewe hufaidiwa nini, ila kuyatazama kwa macho yake tu?

12. Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au kwamba amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.

13. Kuna na balaa mbaya sana niliyoiona chini ya jua, nayo ni hii, mali alizoziweka mwenyewe kwa kujinyima;

14. na mali hizo zimepotea kwa bahati mbaya; naye akiwa amezaa mwana, hamna kitu mkononi mwake.

15. Alivyotoka tumboni mwa mamaye, atakwenda tena tupu-tupu kama alivyokuja; asichume kitu cho chote kwa ajili ya kazi yake, hata akichukue mkononi mwake.

16. Hiyo ndiyo balaa mbaya sana, ya kwamba kama vile alivyokuja, vivyo hivyo atakwenda zake; naye amefaidiwa nini mwenye kujitaabisha kwa ajili ya upepo?

17. Siku zake zote hula gizani, mwenye fadhaa nyingi, mwenye ugonjwa na uchungu.

18. Tazama, mimi niliyoyaona kuwa ndiyo mema na ya kufaa, ni mtu kula na kunywa, na kujiburudisha kwa mema katika kazi yake yote anayoifanya chini ya jua, siku zote za maisha yake alizopewa na Mungu; maana hilo ndilo fungu lake.

19. Tena, kwa habari za kila mwanadamu, ambaye Mungu amempa mali na ukwasi, akamwezesha kula katika hizo, na kuipokea sehemu yake, na kuifurahia amali yake; hiyo ndiyo karama ya Mungu.

20. Kwa kuwa mtu hatazikumbuka mno siku za maisha yake; kwa sababu Mungu humtakabali katika furaha ya moyo wake.

About Mhubiri Chapter 5

Read Mhubiri Chapter 5 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Mhubiri in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Mhubiri
Chapter: 5
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Mhubiri. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Mhubiri Chapter 5 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Mhubiri Chapter 5?

Mhubiri Chapter 5 is part of the Book of Mhubiri in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Mhubiri Chapter 5 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 2
  3. Isaya Chapter 6
  4. Isaya Chapter 14
  5. Isaya Chapter 3
  6. Isaya Chapter 7
  7. Isaya Chapter 8

Explore More from mhubiri

  1. Mhubiri Chapter 1
  2. Mhubiri Chapter 7
  3. Mhubiri Chapter 11
  4. Mhubiri Chapter 4
  5. Mhubiri Chapter 2
  6. Mhubiri Chapter 9
  7. Mhubiri Chapter 10

Related Chapters & Readings

  1. Mambo ya Walawi Chapter 20
  2. 1 Wafalme Chapter 7
  3. Ayubu Chapter 29
  4. Yohana Chapter 20
  5. Nehemia Chapter 5
  6. Zaburi Chapter 34
  7. 1 Samweli Chapter 23
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *