Read Ezekieli Chapter 42 Online
Read Ezekieli Chapter 42 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ezekieli in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Ezekieli and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Ezekieli 42
Sura 42
1. Ndipo akanileta mpaka ua wa nje, njia ya kuelekea upande wa kaskazini; akaniingiza katika chumba kilichopakabili mahali palipotengeka, na kilicholikabili jengo upande wa kaskazini;
2. kukabili urefu wa dhiraa mia palikuwa na mlango wa kaskazini, na upana wake ni dhiraa hamsini.
3. Kukabili zile dhiraa ishirini za ua wa ndani, na kukabili sakafu ya mawe ya ua wa nje, palikuwa na baraza kukabili baraza katika orofa ya tatu.
4. Na mbele ya vile vyumba palikuwa na njia, upana wake dhiraa kumi upande wa ndani, njia ya dhiraa mia, na milango yake ilielekea upande wa kaskazini.
5. Basi vile vyumba vya juu vilikuwa vifupi zaidi; kwa maana baraza zile zilivipunguza kuliko zilivyovipunguza vya chini na vya katikati.
6. Maana vilikuwa vina orofa tatu, wala havikuwa na nguzo kama nguzo za zile nyua; basi kila kilichokuwa cha juu kilikuwa chembamba kuliko cha chini na cha katikati, kutoka chini.
7. Na ukuta ule uliokuwa nje, ubavuni mwa vyumba vile, ulioelekea ua wa nje, kuvikabili vyumba vile, urefu wake ni dhiraa hamsini.
8. Maana urefu wa vyumba vile, vilivyokuwa katika ua wa nje, ulikuwa dhiraa hamsini; na tazama, mbele ya hekalu, dhiraa mia.
9. Na toka chini ya vyumba vile palikuwa na mahali pa kuingilia upande wa mashariki, mtu aviingiavyo toka ua wa nje.
10. Tena palikuwa na vyumba katika unene wa ukuta wa ua, kuukabili upande wa mashariki, kupaelekea mahali palipotengeka, na kulielekea jengo.
11. Nayo njia iliyokuwa mbele yake, kuonekana kwake kulikuwa kama kuonekana kwake vyumba vile vilivyokuwa upande wa kaskazini, urefu ule ule, na upana ule ule; na mahali pake pa kutokea palikuwa sawasawa na vipimo vyake, na sawasawa na milango yake.
12. Na sawasawa na milango ya vyumba, vilivyoelekea upande wa kusini, palikuwa na mlango katika mwisho wa njia ile; yaani, njia iliyoukabili ukuta upande wa mashariki, mtu akiingia.
13. Kisha akaniambia, Vyumba vya upande wa kaskazini, na vyumba vya upande wa kusini, ambavyo vyaelekea mahali palipotengeka, ni vyumba vitakatifu; humo makuhani, wamkaribiao Bwana, watakula vitu vilivyo vitakatifu sana; humo wataviweka vitu vilivyo vitakatifu sana, na sadaka ya unga, na sadaka ya dhambi, na sadaka ya hatia; kwa maana mahali hapo ni patakatifu.
14. Makuhani watakapoingia ndani, hawatatoka mahali patakatifu kwenda hata ua wa nje; lakini wataweka mavazi yao katika mahali wahudumiapo; maana ni matakatifu; nao watavaa mavazi mengine, na kupakaribia mahali palipo mahali pa watu.
15. Basi, alipokuwa amekwisha kuipima nyumba ya ndani, akanileta nje, kwa njia ya lango lililokabili upande wa mashariki, akalipima pande zote.
16. Akaupima upande wa mashariki kwa mwanzi wa kupimia, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote.
17. Akaupima upande wa kaskazini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia pande zote.
18. Akaupima upande wa kusini, mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia.
19. Akageuka aelekee upande wa magharibi, akapima mianzi mia tano, kwa mwanzi wa kupimia.
20. Alipima pande zake zote nne; lilikuwa na ukuta pande zote, urefu wake mianzi mia tano, na upana wake mianzi mia tano, ili kupatenga mahali palipo patakatifu, na mahali palipo pa watu wote.
About Ezekieli Chapter 42
Read Ezekieli Chapter 42 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Ezekieli in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Ezekieli
Chapter: 42
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Ezekieli. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Ezekieli Chapter 42 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Ezekieli Chapter 42?
Ezekieli Chapter 42 is part of the Book of Ezekieli in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Ezekieli Chapter 42 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Habakuki Chapter 3
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- 1 Samweli Chapter 1
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
Explore More from Ezekieli
- Ezekieli Chapter 35
- Ezekieli Chapter 33
- Ezekieli Chapter 37
- Ezekieli Chapter 46
- Ezekieli Chapter 8
- Ezekieli Chapter 21
- Ezekieli Chapter 12