Read Habakuki Chapter 3 Online
Read Habakuki Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Habakuki in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Habakuki and the Holy Bible online.
Choose a Chapter
Habakuki 3
Sura 3
1. Sala ya nabii Habakuki.
2. Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema.
3. Mungu alikuja kutoka Temani, Yeye aliye mtakatifu kutoka mlima Parani. Utukufu wake ukazifunika mbingu, Nayo dunia ikajaa sifa yake.
4. Mwangaza wake ulikuwa kama nuru; Alikuwa na mishale ya nuru ubavuni pake; Ndipo ulipofichwa uweza wake.
5. Mbele zake ilikwenda tauni, Na makaa ya moto yakatoka miguuni pake.
6. Akasimama, akaitetemesha dunia; Akatazama, akawasitusha mataifa; Na milima ya zamani ikatawanyika; Vilima vya kale vikainama; Miendo yake ilikuwa kama siku za kale.
7. Naliziona hema za Kushani katika taabu; Mapazia ya nchi ya Midiani yakatetemeka.
8. Je! Bwana aliikasirikia mito? Je! Hasira yako ilikuwa juu ya mito, Au ghadhabu yako juu ya bahari, Hata ukapanda farasi zako, Katika magari yako ya wokovu?
9. Uta wako ukafanywa wazi kabisa; Viapo walivyopewa kabila vilikuwa neno thabiti; Ukaipasua nchi kwa mito.
10. Milima ilikuona, ikaogopa; Gharika ya maji ikapita; Vilindi vikatoa sauti yake, Vikainua juu mikono yake.
11. Jua na mwezi vikasimama makaoni mwao; Mbele ya nuru ya mishale yako ilipotapakaa, Mbele ya mwangaza wa mkuki wako umeremetao.
12. Ulikwenda katikati ya nchi kwa ghadhabu; Ukawapura mataifa kwa hasira.
13. Ukatokea kwa ajili ya wokovu wa watu wako, Kwa ajili ya wokovu wa masihi wako; Ukakiponda kichwa cha nyumba ya waovu, Ukiuweka wazi msingi hata mwambani.
14. Ukakichoma kichwa cha mashujaa wake kwa fimbo zao wenyewe; Wakaja kama kisulisuli ili kunitawanya; Kama wakifurahi kuwameza maskini kwa siri.
15. Ukaikanyaga bahari kwa farasi zako, Chungu ya maji yenye nguvu.
16. Nikasikia, na tumbo langu likatetemeka, Midomo yangu ikatikisika kwa sauti ile; Ubovu ukaingia mifupani mwangu, Nikatetemeka katika mahali pangu; Ili nipate kuingoja ile siku ya dhiki, Kundi lao washambuliao wakweapo juu ya watu.
17. Maana mtini hautachanua maua, Wala mizabibuni hamtakuwa na matunda; Taabu ya mzeituni itakuwa bure, Na mashamba hayatatoa chakula; Zizini hamtakuwa na kundi, Wala vibandani hamtakuwa na kundi la ng'ombe;
18. Walakini nitamfurahia Bwana Nitamshangilia Mungu wa wokovu wangu.
19. YEHOVA, aliye Bwana, ni nguvu zangu, Yeye huifanya miguu yangu kuwa kama ya kulungu, Naye ataniendesha katika mahali pangu palipoinuka.
About Habakuki Chapter 3
Read Habakuki Chapter 3 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Habakuki in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.
Book Information
Book: Habakuki
Chapter: 3
Testament: Old Testament
How to Read this Chapter
Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Habakuki. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.
More Resources
Continue Reading the Bible
Continue reading Habakuki Chapter 3 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.
Frequently Asked Questions
What is Habakuki Chapter 3?
Habakuki Chapter 3 is part of the Book of Habakuki in the Holy Bible.
Can I read this chapter online?
Yes. You can read the complete Habakuki Chapter 3 online for free with easy chapter navigation.
More Chapters from Agano la Kale
- Zaburi Chapter 1
- Ayubu Chapter 1
- Zaburi Chapter 2
- Ayubu Chapter 4
- Kutoka Chapter 11
- Kutoka Chapter 2
- 1 Samweli Chapter 1