Isaya Chapter 55

For English

Read Isaya Chapter 55 Online

Read Isaya Chapter 55 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Isaya in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Isaya and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Isaya 55

Sura 55

1. Haya, kila aonaye kiu, njoni majini, Naye asiye na fedha; njoni, nunueni mle; Naam, njoni, nunueni divai na maziwa, Bila fedha na bila thamani.

2. Kwani kutoa fedha kwa ajili ya kitu ambacho si chakula? Na mapato yenu kwa kitu kisichoshibisha? Nisikilizeni kwa bidii, mle kilicho chema, Na kujifurahisha nafsi zenu kwa unono.

3. Tegeni masikio yenu, na kunijia; Sikieni, na nafsi zenu zitaishi; Nami nitafanya nanyi agano la milele, Naam, rehema za Daudi zilizo imara.

4. Angalieni, nimemweka kuwa shahidi kwa kabila za watu; kuwa kiongozi na jemadari kwa kabila za watu.

5. Tazama, utaita taifa usilolijua, na taifa lisilokujua wewe litakukimbilia, kwa sababu ya Bwana, Mungu wako, na kwa ajili yake Mtakatifu wa Israeli; maana amekutukuza.

6. Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu;

7. Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; Na amrudie Bwana, Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.

8. Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana.

9. Kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

10. Maana kama vile mvua ishukavyo, na theluji, kutoka mbinguni, wala hairudi huko; bali huinywesha ardhi, na kuizalisha na kuichipuza, ikampa mtu apandaye mbegu, na mtu alaye chakula;

11. ndivyo litakavyokuwa neno langu, litokalo katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.

12. Maana mtatoka kwa furaha, Mtaongozwa kwa amani; Mbele yenu milima na vilima vitatoa nyimbo; Na miti yote ya kondeni itapiga makofi.

13. Badala ya michongoma utamea msunobari, Na badala ya mibigili, mhadesi; Jambo hili litakuwa la kumpatia Bwana jina, Litakuwa ishara ya milele isiyokatiliwa mbali.

About Isaya Chapter 55

Read Isaya Chapter 55 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Isaya in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Isaya
Chapter: 55
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Isaya. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Isaya Chapter 55 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Isaya Chapter 55?

Isaya Chapter 55 is part of the Book of Isaya in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Isaya Chapter 55 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 9
  3. Isaya Chapter 7
  4. Isaya Chapter 13
  5. Isaya Chapter 6
  6. Isaya Chapter 5
  7. Isaya Chapter 3

Explore More from Isaya

  1. Isaya Chapter 37
  2. Isaya Chapter 47
  3. Işaýa Chapter 39
  4. Isaya Chapter 6
  5. Isaya Chapter 59
  6. Isaya Chapter 4
  7. Isaya Chapter 15

Related Chapters & Readings

  1. Isaya Chapter 59
  2. 1 Wakorintho Chapter 15
  3. Mathayo Chapter 7
  4. Mwanzo Chapter 22
  5. Hosea Chapter 4
  6. Zaburi Chapter 141
  7. Mithali Chapter 26
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *