Isaya Chapter 26

For English

Read Isaya Chapter 26 Online

Read Isaya Chapter 26 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Isaya in the Old Testament. Browse every verse with easy chapter navigation, continue to the next chapter, or explore the complete Book of Isaya and the Holy Bible online.

Choose a Chapter

Isaya 26

Sura 26

1. Siku ile wimbo huu utaimbwa katika nchi ya Yuda; Sisi tunao mji ulio na nguvu; Ataamuru wokovu kuwa kuta na maboma.

2. Wekeni wazi malango yake, Taifa lenye haki, lishikalo kweli, liingie.

3. Utamlinda yeye ambaye moyo wake umekutegemea Katika amani kamilifu, kwa kuwa anakutumaini.

4. Mtumainini Bwana siku zote Maana Bwana YEHOVA ni mwamba wa milele.

5. Kwa kuwa amewashusha wakaao juu, Mji ule ulioinuka, aushusha, Aushusha hata nchi, auleta hata mavumbini.

6. Mguu utaukanyaga chini, Naam, miguu yao walio maskini, Na hatua zao walio wahitaji.

7. Njia yake mwenye haki ni unyofu; Wewe uliye mnyofu wainyosha njia ya mwenye haki.

8. Naam, katika njia ya hukumu zako Sisi tumekungoja, Ee Bwana; Shauku ya nafsi zetu inaelekea Jina lako na ukumbusho wako.

9. Kwa nafsi yangu nimekutamani wakati wa usiku; Naam, kwa nafsi yangu ndani yangu nitakutafuta mapema; Maana hukumu zako zikiwapo duniani, Watu wakaao duniani hujifunza haki.

10. Mtu mbaya ajapofadhiliwa, Hata hivyo hatajifunza haki; Katika nchi ya unyofu atatenda udhalimu, Wala hatauona utukufu wa Bwana.

11. Bwana, mkono wako umeinuliwa, lakini hawaoni; lakini watauona wivu wako kwa ajili ya watu wako, nao watatahayari; naam, moto utawala adui zako.

12. Bwana, utatuamuria amani; maana ni wewe pia uliyetutendea kazi zetu zote.

13. Ee Bwana, Mungu wetu, mabwana wengine zaidi ya wewe wametumiliki; lakini kwa msaada wako peke yako tutalitaja jina lako.

14. Wao wamekufa, hawataishi; wamekwisha kufariki, hawatafufuka; kwa sababu hiyo umewajilia, na kuwaangamiza, na kuupoteza ukumbusho wao.

15. Umeliongeza hilo taifa, Bwana, umeliongeza taifa; wewe umetukuzwa, umeipanua mipaka yote ya nchi hii.

16. Bwana, katika taabu zao walikwenda kwako; waliomba maombi mengi wakati adhabu yako ilipokuwa juu yao.

17. Kama vile mwanamke mwenye mimba anayekaribia wakati wake wa kuzaa, alivyo na utungu na kulia kwa sababu ya maumivu yake, ndivyo tulivyokuwa sisi mbele zako, Ee Bwana.

18. Tumekuwa na mimba, tumekuwa na utungu, tumekuwa kana kwamba tumezaa upepo; hatukufanya wokovu wo wote duniani, wala hawakuanguka wakaao duniani.

19. Wafu wako wataishi, maiti zangu zitafufuka; amkeni, kaimbeni, ninyi mnaokaa mavumbini, kwa maana umande wako ni kama umande wa mimea, nayo ardhi itawatoa waliokufa.

20. Njoni, watu wangu, ingia wewe ndani ya vyumba vyako, ukafunge mlango nyuma yako ujifiche kitambo kidogo, mpaka ghadhabu hii itakapopita.

21. Kwa maana, tazama, Bwana anakuja kutoka mahali pake, ili kuwaadhibu wakaao duniani, kwa sababu ya uovu wao; ardhi nayo itafunua damu yake, wala haitawafunika tena watu wake waliouawa.

About Isaya Chapter 26

Read Isaya Chapter 26 online from the Holy Bible. This chapter is part of the Book of Isaya in the Old Testament. Continue reading with the chapter navigation above or explore the complete book.

Book Information

Book: Isaya
Chapter: 26
Testament: Old Testament

How to Read this Chapter

Use the Previous and Next Chapter buttons to continue reading Isaya. You can also adjust the font size for comfortable reading and browse other books of the Bible using the navigation links.

https://www.youtube.com/watch?v=rzsT_Q3KLzE

More Resources

Continue Reading the Bible

Continue reading Isaya Chapter 26 and explore every book, chapter and verse of the Holy Bible. Use the navigation links above and below to move through the Scriptures with ease.

Frequently Asked Questions

What is Isaya Chapter 26?

Isaya Chapter 26 is part of the Book of Isaya in the Holy Bible.

Can I read this chapter online?

Yes. You can read the complete Isaya Chapter 26 online for free with easy chapter navigation.

More Chapters from Agano la Kale

  1. Isaya Chapter 1
  2. Isaya Chapter 13
  3. Isaya Chapter 9
  4. Isaya Chapter 7
  5. Isaya Chapter 5
  6. Isaya Chapter 3
  7. Isaya Chapter 14

Explore More from Isaya

  1. Isaya Chapter 29
  2. Isaya Chapter 18
  3. Isaya Chapter 15
  4. Isaya Chapter 55
  5. Isaya Chapter 7
  6. Isaya Chapter 24
  7. Isaya Chapter 1

Related Chapters & Readings

  1. Zaburi Chapter 63
  2. Kutoka Chapter 23
  3. Ezra Chapter 2
  4. Matendo ya Mitume Chapter 3
  5. 1 Mambo ya Nyakati Chapter 17
  6. Amosi Chapter 1
  7. 1 Timotheo Chapter 5
Share Your Love

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *